Tuesday, July 5, 2016

 Julius Mtatiro: Kwa Uwazi Kabisa Nasema Hii ni AIBU KUU Kwa Taifa la Tanzania
Tunatangaziwa kwa mbwembwe kuwa Taifa letu linaenda kujifunza Teknolojia kutoka Rwanda. So shameful! Taifa ambalo limeshiriki kupigania uhuru wa nchi karibia zote za Afrika. Taifa lenye mamia ya MAPROFESA na wataalamu wa Teknolojia za kila namna. Kwa hiyo hawa MAPROFESA wetu tunaowalipa mamilioni ya mishahara kwa mwezi, tena waliosomea teknolojia mbalimbali Uchina, Urusi, Marekani, Ujerumani, Uingereza na kwingineko (kwenye vyuo vinavyoheshimika duniani) ni Maprofesa UCHWARA! Tatizo la nchi hii ni kubwa hadi mkuu wetu hajua tutaanzia wapi. Kwa uwazi kabisa nasema hii ni AIBU KUU!
Mtatiro J

<meta name="propeller" content="2fc3eb0573476ec843ed3750cc0fd772" />

Saturday, July 2, 2016

 Tamko la RC Makonda kuhusu mashoga waliopo jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza vita na makaka poa (mashoga) na madada poa (makahaba) walioko jijini Dar es Salaam kuwa utaendeshwa msako mkali wa kuwaondoa.

Mkuu wa Mkoa huyo aliyasema hayo kufuatia hali ya vitendo hivyo visiyokubalika na jamii kuzidi kushamiri na kuwa kuna hatari kubwa ya watoto wadogo kuiga vitendo hivyo vinavyoleta picha mbaya kwani ni kinyume na maadili ya mtanzania.

Aidha alisema hawezi kuifumbia macho hali hii kwani inamomonyoa maadali ya jamii na kuwa yuko tayari kulivalia njuga suala hili ili kuhakikisha anawamaliza wote mkoani

Sakati hili la ushoga na ukahaba limeibuka siku za hivi karibuni baada ya kituo cha televisheni cha Clouds Tv kumhoji shoga mmoja ambapo jamii ilipinga kitendo hicho na kuona kama walikuwa wakiuhalalisha ushoga na kuaminisha jamii kuwa ni kitu kizuri.

Friday, July 1, 2016

Nilivyofanya Bonge la Sherehe Baada ya Mke Wangu Kufukuzwa Kazi


Huyu mke nilimuoa akiwa hana kitu, kwa bahati alitafutiwa kazi na ndugu yake kwenye kampuni moja ya simu akawa analipwa kama milioni 3 kwa mwezi fasheni na yeye yeye na fasheni vipodozi kila aina,handbag na nywele za laki mbili ndio mshahara wake ukawa unaishia huko mimi mshahara wangu hauzidi laki sita,nilifanyishwa vituko vyote ndani ya nyumba ,manyanyaso yote ,hapiki hafui,hafanyi chochote ndoa ikawa inaelekea kuvunjika.

Nikaenda mahakamani kuprocess talaka wakasema mpaka nianzie baraza la usuluhishi la kata au kanisani,nikaamua kwenda kanisa tulilofungia ndoa tukaitwa kwa Baba Paroko for hearing sijui mediation sijui arbitration sijui mie nikatinga kwa bajaj ya kukodi nimepaukaaa yeye akaja na RAV4 .
Baba Paroko alivyotusikiliza akaaniita pembeni akasema kijana hapa nadhani hata tukiomba na kukariri mistari yote ya biblia plus mapambio yote ndoa yako haitarudi kama mwanzo pambana utafute hela ,huyu ni mchaga katumwa pesa mjini

Nilisali sana nikasugua goti nikamuomba Mungu mara mambo yangu yakakaa sawa mshahara ukawa mara mbili plus marupurupu anagalau . baada ya miezi miwili sina hili wala lile mara simu yangu nilishangaa mke wangu kunipigia mchana ,tumeachishwa kazi kmpuni imeuzwa,hureeeeee niliruka ruka kwa furaha sana nikapigia simu washikaji tukaenda kunywa bia na nyama choma mpaka saa sita usiku kabla polisi na makonda hawajatuvamia nilijua ile kazi ndio inaniharibia ndoa na aliipata kibahati hawezi tena kupata kazi kama ile.

Hela yote ya NSSF akajaribu kufanya kila biashara biashara zikabuma mtaji ukakata alijifanya hajui kupika sasa anapika kuliko hata wapishi wa Kempinski,alijifanya sijui hawezi kufua sasa anafua kuliko dobi ,kitandani alijifanya mvivu sasa yuko vizuri kuliko wacheza shoo wa fally ipupa ,RAV4 imepaki tu muda wote ananilelea watoto kwa nini nisimshukuru Mungu

Funzo:
Wanawake Msijisahau sana pale mnapokuwa vizuri kifedha zaidi ya mume

Tuesday, June 28, 2016

Yanga mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara wamepoteza mechi yao ya  pili katika kundi A la kombe la shirikisho Tanzania bara.Yanga ambao walionyesha kandanda safi leo uwanja wa Taifa walikubali kichapo hicho huku wakiwa na wachezaji wao wote wa kulipwa pamoja na mchezaji wao waliomsajili hivi karibuni Obrey Cholla Chirwa kwa gharama kubwa.

    Ushindi huo umewafanya TP Mazembe kufikisha point 6 nakuwa vinara kwenye kundi lao hilo,iliwachukuwa dakika 74 kuweza kupata bao lao hilo moja na la ushindi ambako mlinzi wao raia wa Congo kwa jina Merveille Bope akiifungia Mazembe .Yanga sasa inashika mkia katika kundi hilo.
                                                                                                                                                                       

Hifazi kubwa zaidi ya Gesi ya Helium yagunduliwa Tanzania.

Tanzania ni miongoni mwa mataifa chache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.
Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.

Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.
Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia.

Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.

Mnamo mwaka wa 2010 Mwanfisikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.

Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen.

''Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI'' alisema Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford.
Uwanja wa TAIFA wa furika milango yafungwa saa tano baada ya watu kujaa..
TFF imeeleza kuwa milango ya uwanja huo ilifungwa  saa tano asubuhi kutokana na wingi wa mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo na kuingia moja kwa moja uwanjani.

Hadi kufikia saa 11:53 asubuhi, mashabiki waliokuwa nje ya uwanja hawakuruhusiwa kuingia ndani kufuatia majukwaa kufurika mashabiki, nafasi ya kuingia uwanjani imebaki kwa watu maalumu na Wanahabari pekee ambao wanaingilia mlango mkubwa wa Uwanja wa Taifa wakati ile mingine ikiwa imefungwa.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema walilazimika kufungua milango ya uwanjani mapema tofauti na walivyoeleza awali kutokana na mashabiki kufurika uwanjani kuanzia saa tatu asubuhi.
"Mashabiki walianza kumiminika uwanjani kuanzia saa tatu, hatukuwa na namna zaidi ya kufungua milango ya uwanja muda huo ili kuwapa fursa ya kuingia na kupunguza msongamano," alisema Lucas.
Msinifananishe na mal*ya ambao hawajawai kwenda labor kujifungua...Zari
Nani amemchokoza Zari? Kwasababu kwa kile alichokipost kwenye mtandao wa Snapchat inaonekana ameguswa pabaya na amemind!

Najua unajiuliza kwanini hajapost Instagram – ni kwasababu kwa alichokiandika, povu lake lingekuwa la haja! Snapchat ya kishua, mastaa wako huru kusema chochote na hakuna povu kama mitandao mingine. Amesema nini?

“Na wengine acheni kunifananisha na mal*ya ambao hawajawahi kwenda labour,” aliandika. “Mtoto mmoja tu kwenye labour na watakaonekana kama tikiti maji lililopasuliwa. Acheni!”

“Nikiwa na miaka 35 na watoto wanne, badi mimi ni mrembo mno kunifananisha, naomba.”
Afariki baada ya kuchapwa na wazee wa kimila.
Picha ya Tukio jingine
Mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha Kandashi, wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro, Abedi Akyo (53), amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchapwa viboko na wazee wa kimila kwa tuhuma ya kujihusisha na wizi wa kuku.

Akielezea mazingira ya kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilfred Mutafungwa amedai kuwa Akyo alichapwa viboko 70 na wazee hao wa kimila wa Kimeru na Kimasai.

Mutafungwa amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mwezi uliopita  wakazi wa Kata ya Karansi wilayani hapa  walitoa uamuzi kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60 hadi 70.
Utajiri wa Diamond umefikia shilingi bilioni 8.6
Kumekuwepo na tetesi nyingi kuhusu utajiri wa Diamond umefikia kiasi gani. Hilo ni swali ambalo hajawahi kulijibu kwa uhakika zaidi ya kutoa tu hints na kuwaacha wanaouliza kubaki na majibu yao wenyewe vichwani.

Lakini kupitia kipindi maalum cha kituo cha runinga cha E!TV, E Vip kilichorushwa Jumapili ya June 26, tunaweza kusema walau kwa uhakika staa huyo ana utajiri mkubwa kiasi gani. Diamond ana utajiri wa dola milioni 4 za Kimarekani ambao kwa shilingi ya Tanzania ni zaidi ya bilioni 8.6.

Si kitu kinachoshangaza tena kwa Diamond kutokana na hatua aliyofikia akiwa msanii anayelipwa fedha nyingi zaidi Tanzania kwa sasa. Fedha zake nyingi zinatokana na show zake zisizokauka za ndani na nje ya nchi, mikataba ya ubalozi na matangazo kutoka makampuni kama Vodacom, Cocacola, DSTV na Red Gold. Hivi karibuni alipata deal jingine la kutangaza huduma ya taxi ya Uber.

Pia amekuwa akiingiza fedha nyingi kupitia biashara ya nyimbo zake hasa miito ya simu, malipo ya mirabaha kutoka nchi za jirani kama Kenya bila kusahau biashara za mtandaoni zikiwemo Youtube.

Uwekezaji wake kwenye label ya WCB ni kitu kingine kikubwa ambacho kitaanza kumuingizia fedha nyingi siku za usoni. Hadi sasa amesaini wasanii wanne wakiwemo Rich Mavoko, Raymond, Harmonize na dada yake Queen Darleen.

Lakini pia staa huyo anafahamika kwa kuwekeza zaidi fedha kwenye ardhi na nyumba huku akidaiwa kumiliki maeneo mengi jijini Dar es Salaam.